Jumamosi, 8 Aprili 2017

Msanii Roma Mkatoliki anadaiwa kupatikana na yupo Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar

Msanii Roma Mkatoliki anadaiwa kupatikana na yupo Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar

.

Habari ya akina Roma kupatikana imethibitishwa na Mkurugenzi wa Tongwe Records J. Mada.

Bado hakuna maelezo ya kutosha kuhusiana na wapi walipokuwa na nani waliokuwa wamewashikilia. Kwa sasa wanadaiwa kuwepo kituoni hapo kwa taratibu za kipolisi kwa kuwa jalada la kupotea kwao lilifunguliwa hapo.

Kupatikana kwao kumefuatia wito mkubwa uliokuwa ukipaishwa na wasanii wenzake na mashabiki kuhusu kuachiliwa huru, ndani na nje ya mitandao ya kijamii.

Awali, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishina Simon Sirro alisema bado walikuwa wakiendelea na upelelezi wa tukio la kupotea (kutekwa) kwa msanii Roma Mkatoliki na wenzake.

Taarifa zaidi zinafuata