Ijumaa, 7 Aprili 2017

Je,wajua madhara ya kutenda dhambi ya uzinzi au uasherati hata ukitubu na kusamehewa? Soma hapa..

*KUHUSU_SEX..*

*_NI KWELI UTATUBU LAKINI MAMBO HAYA YATABAKI KWAKO DAIMA...!_*👇👇

Vijana wengi sasa (waliokoka) wana fanya SEX wakat wa mahusiano (kabla ya ndoa), na huku Mioyoni mwao wanasema tukifanya Tutatubu.

Ni kweli utatubu na kama Toba yako ni ya KWELI Mungu Atakusamehe lakini mambo haya hayataondoka hata kama Utatubu..

✴HOFU YA MUNGU KUPUNGUA.

Kwa mara ya kwanza kabla mtu hajafanya sex, huwa na Hofu Moyoni mwake kuhusu dhambi hiyo na Hofu hii humfanya ajilinde na kujitunza.

Lakini Baada ya kufanya Sex, ile Hofu huondoka na badala yake swala la kuvua Nguo linakuwa ni jambo la kawaida tu.

✴KUMBUKUMBU KUBAKI KICHWANI.

Ukishafanya sex, utatubu lakini kuna muda yale matukio ya tendo hilo yatakuwa yanarudi kwenye ufahamu wako mara kwa mara.

Kumbukumbu hizi huwa hazifutiki na ndio maana wengi hujikuta wakizini tena baada ya KUTUBU.

✴UJASIRI WA KUFANYA UONGEZEKA.

Mtu aliyefanya uzinzi ni rahisi zaidi kurudia kufanya tena, Ukweli ni kwamba lile tendo lina Raha ila ubaya unakuja tu pale linapofanyika kinyume na UTARATIBU.

Na kwa sababu ulifanya ukatubu, na haukuona madhara yoyote yaliyokupata zaidi ya Burudani uliyopata hivyo unaona urudie Tena, kujipa raha Zaidi.

Lakini Biblia inasema mshahara wa dhambi ni MAUTI (Warumi 6 :23).

✴KUKOSA NGUVU YA KUJIZUIA.

Baada ya kufanya Sex, Nguvu ya kujizuia USIFANYE tena hupungua na yamkini kufa kabisa.

Tangia hapo utakuwa ni mtu wa kuanguka na kasimama, kuanguka na kusimama. Unakuwa sawa na mji usio na Ukuta, nyumba isiyo na milango mwizi ni RAHISI kuingia au sawa na gari linalotembea bila ya Brake.

Ni wachache sana waliofanya halafu wakasimama kikamilifu bila kuanguka tena hasa pindi wanapokuwa kwenye uhusiano ambao unawafanya wakutane mara kwa mara.

✴KUMBUKUMBU KUBAKI VICHWANI MWA WATU.

Unapoanguka kwenye dhambi ya UZINZI na watu wakafahamu basi dhambi hiyo haitafutika Katika FIKRA za watu hata Ukifa.

Mpaka Leo tunasoma dhambi ya Daudi alipozini na mke wa Uria, ingawa Daudi alitubu, akasemehewa na TAYARI ameshakufa lakini dhambi hiyo bado ipo HAI inaishi kwenye vichwa vyetu na mpaka kwa wajukuu zetu bado watasoma na kusikia dhambi hiyo.
..............................................

Mbali na Mimba, mgonjwa ya zinaa na kupoteza Ujana Wako (bikira) Baada ya kufanya Sex, hayo tuliyoona ni MADHARA ya KUDUMU ambayo huweka KOVU Katika Maisha yako *LISILOFUTIKA*.

...................................................

 *_"Mtu AZINIYE na mwanamke (/mwanaume) HANA AKILI KABISA, afanya jambo LITAKALOMWANGAMIZA Nafsi yake._*

*_'Atapata Jeraha na KUVUNJIWA heshima, wala FEDHEHA yake HAITAFUTIKA."_*

         _MITHALI 6 : 32-33_

*_"Ikimbieni ZINAA, kila dhambi atendayo mwanadamu ni NJE ya Mwili wake, ila yeye afanyaye ZINAA hutenda JUU YA MWILI WAKE MWENYEWE "_*

      _1 WAKORINTHO 6 : 18_