Jumapili, 2 Aprili 2017

Vikosi vya kagera sugar vs simba hivi hapa


Klabu ya Simba leo inamkosa beki wake wa kulia Javier Bukungu katika mchezo wa ligi kuu unaoanza muda mfupi ujao dhidi ya Kagera Sugar katika dimba Kaitaba Bukoba, kwa mujibu wa kikosi kilichowekwa hadharani hivi punde.
Kikosi cha Simba
Katika kikosi kitakachoanza, nafasi ya Bukungu itachezwa na kiungo James Kotei huku idara nyingine zikionekana kutobadilika ambapo Mzamiru Yasin atasaidiana na Jonas Mkude katikati, huku Ndemla akisogea mbela kusaidia na Ibrahim Ajibu katika safu ya ushambuliaji.
Katika safu ya ulinzi wa kati, siku ya leo Juuko Murshid atasaidiana na Abdi Banda wakati viungo wa pembeni wakiwa ni Ibrahim Ajibu na Shiza Kichuya.
Hiki ndicho kikosi cha Simba
 

Kwa upande wa Kagera Sugar kikosi chake kipo kama kifuatavyo.
Juma Kaseja, Godfrey Taita, Mwaita Gereza, Juma Shemvuni, Mohamed Fakhi, George Kavila, Suleiman Mangoma, Ame Ally ‘Zungu’, Edward Christopher, Mbaraka Yusuph na Japhet Makalai