Utangulizi
Viwavi jeshi (Helicoverpa ssp) ni hatua ya lava wa kipepeo katika ukuaji wake.
Wanakula majani kwa wingi na kusababisha mmea kushindwa kujitengenezea chakula chake kwa ajili ya ukuaji wake.
Ni adui mkubwa kwa mkulima kwa sababu wanashambulia mimea mengi kama mahindi,pamba, mbaazi, dengu, nyanya, mtama , kunde n.k
Wanatabia ya kukua kwa haraka mno kipindi cha kipupwe.
Mzunnguko wa maisha
Ni imani iliyowekwa kwamba vipepeo huishi kwa mda mfupi sana kuanzia wiki moja hadi takribani mwaka mmoja kulingana na maisha yao hivyo ni muhimu kujua hatua za mdudu huyu ili kutusaidia kutambua ni hatua ipi ambayo hushambulia mazao yetu na kutafuta njia sahihi ya kudhibiti ili asiendelee kuharibu mazao yetu.
Mzunguko una sehemu 4 ambazo ni;
Yai
Kipepeo anauwezo wa kutaga mayai (fertile eggs) kwenye majira ya baridi (kipupwe) siku 6 hadi10 na kwa upande kiangazi (25°C) ndani ya siku 3.
Kiwavi (lava)
Kiwavi wa kipepeo hula majani kwa wingi na hutumia mda wao wingi kutafuta chakula na wachache wao hula wadudu, kiwavi anapitia instar 6 na kukamilisha ukuaji wake ndani ya wiki 2 hadi wiki ya 3 wakati wa kiangazi au ndani ya wiki ya 4 hadi 6 kipindi cha masika. Na kwenye hatua hii viwavi jeshi huwa wanauwezo wakuzalisha kimekali fulani na kutumika kama ulinzi kwao.
Hii ni hatua hatari sana kwa mkulima kwa sababu ni hatua ambayo viwavi jeshi wanakula majani na kushambulia zaidi sehemu nyingine muhimu za mmea kama podi,mbegu ,maua, machipukizi ya mmea, na matunda. Ni muhimu kujua 90% ya uharibifu unafanywa na hatua hii kuanzia instar ya 3 na kuendelea.
Bundo (pupa)
Kiwavi anapokuwa na kukamilika, kuna homoni kadhaa huanza kuzalishwa wakati huu, kiwavi huacha kula na kuanza kutafuta sehemu na kutulia mara nyingi huwa chini ya majani. Hatimaye kiwavi hubadika kuwa bundo. Bundo kwa kawaida hajongei na isipokuwa huweza kujitikisa au kujinyonga nyonga na kutoa milio kadhaa kuwatishia wadudu. Hii hutokea ndani ya wiki 2 kwa upande wa kiangazi na wiki 6 kwa upande wa masika.
Ndumili (imago)
Baadae bundo hukua na kupitia mabadiliko katika mfumo wa metamofosisi na kuwa kipepeo kamili.katika hatua hii kipepeo huitwa ndulimi. Hii hatua hukamika ndani ya siku 10.
Jinsi ya kudhibiti
1.Nyunyuzia dawa ya kuua wadudu mfano
cypermethrin, deltamethrin, chlorpyrifos, dicofol, triazophos, thiodicarb, methomyl
2.Fanya mzunguko wa mazao (crops rotation). Usipande zao sehemu moja kila msimu
3.Unatakiwa kutumia mbegu safi na bora
Panda mbegu zinazohimili ugonjwa
4.Teketeza masalia ya mimea
Home
Unlabelled
Jumatatu, 13 Machi 2017

Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Matokeo ya utafutaji
Followers
Popular Posts
-
*KUHUSU_SEX..* *_NI KWELI UTATUBU LAKINI MAMBO HAYA YATABAKI KWAKO DAIMA...!_*👇👇 Vijana wengi sasa (waliokoka) wana fanya SEX wakat wa...
-
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali kwa kushirikiana na kampuni ya Viettel ya Vietnam inatekeleza mradi wa ujenzi wa miundombinu ...
-
Bungeni: Waajiri Na Waajiriwa Zingatieni Sheria Za Kazi Kuondoa Migogoro Kazini: Majaliwa Na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma. Wa...
EmoticonEmoticon