Kipindi cha Pili kimeanza Taifa stars wameanza mechi kwa nguvu.
Kadri mechi inavyoendelea Burundi wanabadilika na Taifa stars wasipokuwa makini watapa taabu kuwazuia hawa warundi.
Mavugo anaipatia Burundi bao la kwanza sasa ni bao 1-1
Wachezaji wa Burundi wakishangilia bao lililofungwa na Mavugo.
Mechi sasa imechangamka warundi nao sasa wameamka wanaonesha kabumbu safi.
Ubinafsi wa msuva unaendelea kuwatesa stars.mabadiliko yaliyofanyika kwa stars bado hayajazaa matunda Hajib hajaonesha uwezo wake.
Shambulizi la dk 77 ,Mbaraka Abeid Yusuph anaipatia stars bao la 2 Tanzania vs Burundi 2-1 dk 77
Mbaraka Yusuph ikiwa mechi yake ya kwanza ya timu ya Taifa anafunga goli lake la kwanza pia.
Mabadiliko ya kuingia Ndemla ,Mbaraka na Mkude angalau yameleta kashikashi na kupunguza mashambulizi ya Burundi.
Huyu hapa Mbaraka Yusuph aliyefunga goli akishangilia goli
Mechi imemalizika matokeo Taifa stars dhidi ya Burundi 2-1
Asanteni kwa kuendelea kufuatilia na kusoma blog hii.