Askari wawili wa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameuawa na wengine wa 3 kujiruhiwa katika mapigano makali yaliotokea Jumatatu saa za asubui.
Mapigano hayo yalizuka katika mji wa Lubero kilometa 45 kusini mwa mji wa Butembo taarifa zasema walioshambulia ni wapiganaji wa Mai Mai wa kundi la LAFRAPA.
Jeshi la Congo limesema hata hivyo hali imerudi kuwa tulivu kwa sasa na wapiganaji hao wakiwa wote wamekimbia kwani Umoja wa Mataifa MONUSCO uliingilia kati.
Wakati huohuo vijana wa vyama vya upinzani na vyama tawala wanakutana Goma kutafakari kuhusu mustakbali wa DRC katika wakati huu mgumu wakutokuwepo uchaguzi.
Akizungmuzana na voa kwa njia ya simu mmoja wa wakazi wa eneo la Lubero alikokuwa amejificha, asema mlio wa silaha ulianza sakumi na moja za asubui.
Taarifa zasema kambi ya jeshi ilichomwa moto na waasi hao na wakati wa mapigano askari wa 2 waliuawa na wengine zaidi ya 3 walipata majeraha ya risasi ila idadi ya waasi haijulilkane.
Kambale Mayani ambaye ni kamanda wa walioshambulia Lubero alizungumza kwa simu akiwa kwenye milima ya Lubero.
Jeshi kwa upande wake limesema kuwa mai mai hao watashughulikiwa ikiwa hawataki kujisalimisha wano na silaha zao na kuacha uvunjifu wa amani.