Jumapili, 16 Julai 2017

KANUNI BORA ZA UFUGAJI WA MBUZI



   KANUNI BORA ZA UFUGAJI WA MBUZI



Mbuzi na kondoo ni wanyama ambao wanaweza kufugwa kwa gharama nafuu pia ni wavumilivu wa ukame na maradhi tofauti na ngo’mbe kwa kua wana umbile dogo wanaweza kufugwa katika eneo dogo na nguvu kazi ndogo na hata kwa wenye kipato kidogo.Kuzaa(uzao) kwa muda mfupi kuna mwezesha mfugaji kuwa na mifugo mingi kwa muda mfupi

Mbuzi na kondoo wanaweza kufugwa kwa ajili ya nyama/maziwa/ngozi/sufi na mazaomengine kwa matumizi ya familia na kuongeza kipato.

NAMNA BORA YA UFUGAJI:-

Wafugwe kwenye banda bora
Chagua kulingana na sifa zao na lengo la ufugaji(uzalishaji)nyama/maziwa/sufi.
Walishwe chakula sahihi kulingana na umri
Kuzingtia ushauri wa mtaalamu wa mifugo hasahasa namna ya udhibiti wa magonjwa.
Kuweka kumbukumbu za uzalishaji.
Kuzalisha nyama/maziwa/sufi bora unaokidhi mahitaji ya soko.

ZIZI AU BANDA LA KONDOO AU MBUZI


Ø Banda bora linatakiwa liwe ni lenye kuweza kuwakinga mbuzi au kondoo na mashambulizi ya wanyama wakali(hatari) na wezi.
Ø Liwepo sehemu ambayo maji hayawezi kutuama.
Ø Mabanda yatenganishwe kulingana na umri.
Ø Liwe na ukubwa ambao linaweza kufanyiwa usafi.

Kama utafuga mbuzi au kondoo kwa kuwafungia(shadidi) muda wote zingatia yafuatayo:-

Ø banda imara lenye uwezo wa kuwahifadhi kiafya,upepo/mvua n.k
Lenye hewa ya kutosha
Liwe na sakafu ya kichanja na sehemu ya kuwekea chakula na maji.
Liwe na vyumba tofauti kwa kuweka vijitoto/wanao ugua/wanao kua.

UJENZI WA BANDA LA MBUZI AU KONDOO

Banda lijengwe kwa kutumia vifaa vilivyopo eneo husika na kwa kuzingatia uwezo wa mfugaji.
Kuta ziwe imara na zinazo ruhusu mwanga na hewa ya kutosha.
Mlango uwe na ukubwa wa 60X150 sentimeta.
Sakafu iwe ya udongo/zege ya kichanja unaweza kutumia mabanzi/mianzi na iruhusu kinyesi na mikojo kudondoka chini
Chumba cha majike na vitoto kiwe na sentimeta 1.25kati ya fito na fito au papi na papi,chumba cha mbuzi/kondoo wakubwa kiwe na sentimeta 1.9kati ya mbao na mbao.

UCHAGUZI WA MBUZI/KONDOO WA KUFUGA:-

Lengo ni kuboresha uzalishaji na kupata kizazi bora kuna aina nyingi za mbuzi/kondoo wa kufugwa kulingana na maingira na mahitaji ya mfugaji.Uchaguzi unaweza kufanyika kuangalia umbile,uzalishaji na kumbukumbu za wazazi kama vile umbo kubwa,ukuaji wa haraka uwezo wa kutunza vitoto na kutoa maziwa mengi,mbuzi wanao faa kwa maziwa ni-:
              i.        saanen,
            ii.        noewegian na
          iii.        toggenburg na chotara wao

Wanaofaa kwa nyama boer ni achotara wao mbuzi wa asili pere white newala na ujiji.Malya (blended)wanafaa kwa maziwa na nyama.

Pia kondoo aina ya black head Persian(bhp),masai red,Suffolk na Hampshire wanafaa kufugwa kwa ajili ya nyama.
Merino na Lincoln hufugwa kwa ajili ya sufu.
Corriedale na Romney hufugwa kwa ajili ya nyama na sufu nchini kwetu kondoo wanaopatikana kwa wingi ni black head Persian,masai red dopper
Kondoo/mbuzi jike wanaofaa kwa kuzalisha maziwa na nyama:-
Historia ya kukua upesi
Kuzaa mapacha
Kutunza watoto


SIFA ZA ZIADA:-

Miguu ya nyuma iliyo nyooka na yenye nafasi kwa ajili ya kiwele,kiwele kiwe kikubwa na chuchu ndefu zilizo kaa vizuri.

SIFA ZA DUME:-


Miguu iliyo nyooka na yenye nguvu
Mwenye kokwa mbili zilizo kaa vizuri a kunyooka
Mwenye uwezo na nguvu za kupanda
Asiwe na ulemavu

UTUNZAJI WA VITOTO:-

Hakikisha kitoto kinapata maziwa ya mwanzo(dang’a)siku ya kwanza-3.
Kama kinanywesha kipewe lita 0.7-0.9 kwa siku maziwa haya ni bora kwa kuwa yana viinilishe na kinga dhidi ya magonjwa
Kama mama hatoi maziwa au amekufa kondoo au mbuzi mwingine anae nyonyesha anaweza kusaidia kukinyonyesha.
Kitoto kinyonye kwa wiki12-16 baada ya wiki2 kuzaliwa pamoja na maziwa apewe chakula kingine kama nyasi ili akuze
tumbo lake pia apewe maji ya kutosha.
Aachishwe kunyonya akifikisha miezi 3
Vipewe chanjo ya magonjwa kulingana na ushauri wa mtaalam


MATUNZO MENGINE:-

Mbuzi au kondoo awekewe alama aili iwe rahisi kwa mfugaji kutunza kumbukumbu.

KUONDOA VISHINA VYA PEMBE:-

Aondolewe vishina kati ya siku 3-14 na mtaalam wa mifugo
KUHASI:-Vitoto ambavyo havitatumika kuendeleza kizazi vihasiwe na mtaalam wa mifugo

UTUNZAJI WA MBUZI/KONDOO WA MIEZI4-8:-

Ili kondoo/mbuzi aweze kukua na kupevuka mapema zingatia mambo yafuatayo:-

Kumpatia chakula cha ziada kwa miezi 2 mfululizo kiasi cha kilo0.2-0.7 kwa siku kuanzia anapo achishwa kunyonyesha.
Kumpatia dawa za kuzuia minyoo kama iatakavyo shauriwa na mtaalam wa mifugo na aogeshwe mara kwa mara ili kuzuia magonjwa.
Kukata kwato zikikomaa.

UMRI WA KUPANDISHA:-

Wakitunzwa vizuri wanaweza kupandishwa wakiwa na umri wa miezi 8-12 kwa walioboreshwa miezi18-24 kwa mbuzi wa asili iatategemea na afya alonayo pia inashauriwa apandishwe akiwa na uzito wa kilo 12.

DALILI ZA JOTO:-

Hutingisha mkia
Hutoa ute mweupe ukeni
Hufuata dume
Hamu ya kula hupungua
Hukojoa mara kwa mara
Uke huvimba na huwa mwekundu kukiko kawaida
Huangaika mara kwa mara na kupiga kelele
Kwa mbuzi anayekamuliwa hupunguza kiwango cha maziwa.
Mbuzi/kondoo mwenye dalili hizi apelekwe kwa dume na uchunguze tena dalili za joto baada ya siku 19-21
Msimu mzuri wa kuzaa ni baada ya mvua.

UTUNZAJI WA MBUZI/KONDOO MWENYE MIMBA:-

Mbuzi hubeba mimba kwa muda wa miezi 5
Apewe chakula cha ziada 0.2-0.7.
Apewe nyasi,miti malishi na mikunde mchanganyiko kilo 1.8-2.5 kwa siku

DALILI ZA KUKARIBIA KUZAA:-

Huangaika kwa kulala na kuamka mara kwa mara
Hujitenga na kundi na hufuata sehemu kavu na yenye kivuli
Hutokwa na ute mzito ukeni
Hupiga kelele
Pindi ukiona dalili hizi muandalie sehemu maalum ya kuzalia na muwekee maji ya kutosha.

UTUNZAJI WA MBUZI/KONDOO ANAYE NYONYESHA:-

Huhitaji chakula zaidi kwa kuzalisha maziwa na chakula ya kitoto pamoja na nyasi,mikunde na majani ya miti malisho kilo 1.8-2.5 kwa siku ni muhimu apewe nyongeza ya 0.3-0.8 kwa kila lita inayoongezeka na maji safi na slama wakati wote

UKAMUAJI WA MAZIWA:-

Sehemu ya kukamulia safi na tulivu.
Awe na afya nzuri,msafi kiwele kioshwe na maji safi ya uvuguvugu.
Mkamuaji asibadilishwe badilishwe,awe msafi mwenye kucha fupi na asiwe na magonjwa ya kuambukiza.
Vyombo vya kukamulia view safi.
Maziwa ya mwanzo yakamuliwe kwenye chombo malum(strip cup)kwa uchunguzi wa ugonjwa wa kiwele.

UTUNZAJI WA DUME BORA LA MBEGU:-

Dume la mbegu linahitaji matunzo mazuri ili litoe mbegu bora kupanda na kuzalisha.
Dume bora huanza kupanda akiwa na miezi 8-10 msimu wa kupandisha dume 1 lipandishwe majike 40-50 inashuriwa madume yenye miezi 8-9 yapandishwe majike ambayo ni mara ya kwanza kupandwa.
Malisho ya kutosha na chakula cha ziada kisipungue kilo 0.2-0.7 kila siku na maji ya kutosha.
Majani ya miti yenye lishe,mikunde na nyasi na mabaki ya mazao pia kilo 0.45-0.9 za chakula cha ziada kulingana na uzito wake na wingi wa majike anayopanda wiki 2 kabla