HESHIMA KATIKA JAMII YAKO
Ndio maana utakuta kuna watu wanatumia pesa au mbinu nyingi sana kuweza kujenga heshima. Hali hiyo yote inaonyesha kwamba heshima ni mojawapo ya kitu cha thamani na kinachokubalika sana katika jamii yoyote ile.
Pamoja na umuhimu wa heshima kwa wengi, sasa kitu ambacho tunatakiwa tujiulize mimi na wewe ni kwamba, je, kati yetu ni wangapi hasa wanajua namna ya kujenga heshima zao katika jamii?
Je, pesa peke yake ndio ina uwezo wa kujenga heshima? Au ni kitu gani ambacho unatakiwa uwe nacho ili kikusaifdie kuweza kujenga heshima kubwa katika jamii na kujikuta ukikumbukwa pengine vizazi na vizazi?
Kama nia yako ni kutaka kujenga heshima na ukawa mtu wa kuheshimika, fahamu mambo haya;-
1. Toa thamani.
Ili uweze kujenga heshima kubwa kwa jamii inayokuzunguka, toa thamani, fanya vitu ambavyo vinagusa maisha ya watu. Haijalishhi unafanya kitu gani lakini lilokubwa fanya kitu ambcho kinagusa maisha ya watu, kina mchango wa kubadili maisha ya wengine.
Siku zote haijalishi una pesa za kiasi gani, lakini je, kupitia hizo pesa wewe binafsi unatoa mchango gani kwa wengine kufanya maisha ya yakabadilika? Watu wote wanaotoa thamani na kuweza kubadili maisha ya wengine ni watu wa kuheshimika.
Kama unafikiri natania kuhusu hili angalia watu waliokuwa wakipagania uhuru, heshima zao zikoje katika jamii zao, utangudua heshima zao ni kubwa sana. Hivyo hiyo inatuonyesha njia mojawppo ya kujiwekea heshima toa thamani kwa kugusa maisha ya watu.
2. Wakubali watu.
Mbali na kutoa thamani, njia mojawapo nyingine ambayo inaweza kukujengea heshima ni kuwakubali watu. Kubali mawazo yao wanayotoa ila kama kweli yanasaidia kujenga jamii au kuwasaidia wengine.
Kama unahitaji kuwakosea, tafadhari usiwakosoe hadhari, jitahidi ukosoe kwa pembeni. Hiyo pia ni njia nzuri ya kukusaidia kujua au kutambua kwamba yapo makosa ambayo umeyaona na ni muhimu kurekebishwa.
3. Unapokosea, omba msamaha.
Hakuna mtu ambaye tunaweza tukasema yupo kamili kwa asilimia zote. Hivyo, unapokosea iwe kwa jamii yako au kwa watu wako wa karibu, hebu kuwa mwepesi wa kuomba msahamaha.
Msahama ni kitu kidogo sana lakini utakusaidia kukujengea picha kwa watu wengine kwamba una busara. Kwa sababu ya busara zako utajikuta ukiwa ni mtu wa kuheshimika karibu na watu wote.
Hizi ni mbinu miuhimu ambazo mtu yoyote anayataka kuheshimiak katika jamii yake anaweza akazitumia kama njia mjawapo ya kumsaidia kumjengea heshima kubwa katika jamii yake.