Alhamisi, 4 Mei 2017

Wenger asalia kimya kuhusu mkataba Arsenal

Wenger asalia kimya kuhusu mkataba Arsenal

Hivi ni viunganisho vya nje na vitafungua katika dirisha mpyaMshirikishe mwenzako
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ameendelea kugomea maswali kuhusu mustakabali wake.
Ametania wanahabari kwamba mwenyewe alifanya makosa alipoahidi kwamba atakuwa amefanya uamuzi wake kuhusu mkataba mpya kufikia sasa.
Wenger, 67, amekuwa mkufunzi mkuu wa Gunners tangu 1996 na mkataba wake wa sasa unafikia kikomo mwisho wa msimu huu.
Februari, alitangaza kwamba angeamua kuhusu mkataba mpya machi au Aprili.
Akizungumza kabla ya mechi ya Jumapili kati dhidi ya Manchester United, Mfaransa huyo alitania: "Hii ina maana kwamba nilikosea."
Aliongeza: "Sitaki kuzungumzia kisa hiki changu tena."
Wenger: Arsenal waliwajibu wakosoaji
Baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo waliandamana na kumpinga meneja huyo wa muda mrefu.
Mara kwa mara walianika mabango yenye ujumbe: "Wenger Nje".
Baada ya kuchapwa 2-0 na wapinzani wao wa London Tottenham Hotspur Jumapili, vijana hao wa Wenger wamesalia namabri sita kwenye jedwali na wamo hatarini ya kukosa kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwa mara ya kwanza katika miaka 20.

Arsenal wako nyuma ya Manchester City kwa alama sita, ingawa wana mechi moja hawajacheza.
Hata hivyo, watategemea wapinzani wao wateleze ndipo wapate matumaini ya kumaliza katika nne bora.
"Sasa, kushinda mechi zote zilizosalia hakuwezi kutuhakikishia nafasi ya kufuzu, kusema kweli hatima yetu haimo mikononi mwetu. Lakini lazima tushinde mechi, hilo ndilo pekee tunaweza kufanya," aliongeza Wenger.
"Tulisikitishwa na amtokeo ya wikendi lakini wakati mwingine jambo jema zaidi ni kuwa na mechi kubwa nyingine moja kwa moja na tunataka kurejea kwa kishindo."


EmoticonEmoticon