Ijumaa, 26 Mei 2017

MARUFUKU USAJILI WA KUFURU CHINA



Shanghai, China. Shirikisho la Soka China (CFA), limetangaza sera mpya inayohusiana na gharama za uhamisho kwa wachezaji wa kigeni hasa ikiwalenga wachezaji wanaohusishwa kwenda kucheza ligi nchini humo.
Sera hiyo huenda ikaanza kufanya kazi kwa wachezaji Diego Costa na Pierre- Emerick Aubameyang wanaohusishwa kwenda kucheza Ligi Kuu ya China.
Mchezaji huyo wa Chelsea amewekewa kiwango cha mwisho cha uhamisho ambacho kinatakiwa kisizidi Pauni 60 milioni.
Costa amekuwa akihusishwa kujiunga na klabu ya Tianjin Quanjian wakati naye mchezaji wa Borussia Dortmund amewekewa kiwango hicho hicho.
Wachezaji waliotimkia kucheza soka China ni Oscar, Hulk, Carlos Tevez, Ezequiel Lavezzi, Axel Witsel, Graziano Pelle, Paulinho, Ramires na Alex Teixeira.
“Klabu ambayo ambayo itafanya usajili usajili mkubwa kinyume na sera itatozwa faini” ilisomeka taarifa ya shirikisho hilo.


EmoticonEmoticon