Stand United ipo nafasi ya 11 ikiwa na pointi 27, lakini wakati Liewig anaondoka ilikuwa katika nafasi ya timu nne za juu.
Dar es Salaam. Kocha Patrick Liewig amewambia viongozi wa Stand United wajitathimini kwa mwenendo wa timu yao na kuwashauri kufanya mambo matano ya kuinusuru timu hiyo.
Stand United ipo nafasi ya 11 ikiwa na pointi 27, lakini wakati Liewig anaondoka ilikuwa katika nafasi ya timu nne za juu.
Liewig aliyevunja mkataba na Stand United mwanzoni mwa msimu huu na kuiacha timu hiyo katika nafasi ya juu kwenye msimamo amebainisha kuendelea kufuatilia mwenendo wa timu hiyo licha ya kuondoka.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya email, Liewig ameshangazwa na kupotea katika ushindani kwa Stand United, lakini akaishauri na kusema kama itafanikiwa kubaki Ligi Kuu msimu ujao irekebishe kasoro tano ili iimarike kiushindani.
"Naipenda Stand na nilifanya nao kazi vizuri kabla ya kushindwana katika maslahi, natamani kuiona inaendelea kucheza Ligi Kuu.
"Lakini ifanye haya kama kweli inahitaji kurudi kwenye ushindani, suala la nidhamu lipewe kipaumbele cha kwanza kwenye timu.
"Benchi la ufundi kutopangiwa timu na viongozi, pia kuachiwa kocha afanye usajili anaohitaji na kocha kuepuka kutengeneza makundi kwa wachezaji wake," alisema Liewig.
Kocha huyo Mfaransa alisisitiza kwamba alipokuwa Stand mambo hayo yalikuwepo, lakini alimudu kuyapinga kwa nguvu zote