Ijumaa, 10 Machi 2017

Viwavijeshi vyavamia mashamba Morogoro waaribu mazao wakulima warudia kupanda tena

Viwavijeshi vyavamia mashamba Morogoro


Wadudu aina ya viwavijeshi wamevamia na kuharibu mazao kwenye mashamba yaliyopo katika kata 11 za Wilaya ya Morogoro na kusababisha hofu kwa wakulima.

Diwani wa kata ya Mikese, Mohamed Mzee amesema viwavijeshi hao wameathiri sana mashamba ya mahindi.

Mzee amesema tayari ameshatoa taarifa kwa ofisa ugani wa kata hiyo ili wakulima waweze kupatiwa dawa na utaalamu wa kuua wadudu hao waharibifu wa mazao.

Diwani huyo amesema viwavijeshi hao walianza kuonekana wiki mbili zilizopita kwenye mashamba lakini baada ya mvua kunyesha wameanza kupungua.

Ofisa kilimo wa Wilaya hiyo, Maria Leshalu amekiri kupata taarifa hizo na kusema kuwa tayari alishawasiliana na maafisa ugani wa kata na kuwataka kuandaa taarifa ya hali ya uharibifu na maeneo yaliyoathirika