Alhamisi, 23 Machi 2017

Nape Nnauye amwagiwa sifa na kiongozi wa chama cha upinzani Tanzania

Nape Nnauye amwagiwa sifa na kiongozi wa chama cha upinzani Tanzania.

Nnape NauyeHaki miliki ya pichaNNAPE NAUYE/TWITTER
Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo nchini Tanzania Zitto Kabwe amesema waziri wa habari aliyefutwa kazi Bw Nape Nnauye "ni shujaa".
Taarifa kutoka ikulu mapema leo ilitangaza waziri mpya wa habari, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwa Dkt. Harrison George Mwakyembe.
Taarifa hiyo haikusema chochote kuhusu hatima ya Bw Nnauye.
Bw Nnauye kwenye Twitter amewaomba watu kuwa na subira na kuahidi kwamba atazungumza na wanahabari baadaye leo.
"Ndugu zangu naomba TUTULIE! LEO mchana nitakutana na Wanahabari na tutalizungumza hili. Nitawaambia saa na mahali, kwasasa naomba TUTULIE!" ameandika.
Baadaye taarifa zilianza kuibuka kwamba Bw Nnauye alikuwa amekamatwa, lakini mwanasiasa huyo aliandika kwenye Twitter kwamba bado hajakamatwa na yupo salama.
NnauyeHaki miliki ya pichaTWITTER
Kwenye Twitter, Bw Kabwe, ambaye ni mbunge wa Kigoma-Ujiji Municipality amesema aliwasiliana na Bw Nnauye ambaye amemthibitishia kwamba ni kweli ameondolewa kwenye wadhifa wake wa uwaziri.
KabweHaki miliki ya pichaTWITTER
Dkt Mwakyembe amekuwa akihudumu kama Waziri wa Katiba na Sheria.
Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) limempongeza Dkt Mwakwembe kufuatia uteuzi wake.
NauyeHaki miliki ya pichaTWITTER


EmoticonEmoticon