Jumamosi, 18 Machi 2017

Mashabiki wa Arsenal wamjia juu Arsene Wenger wamtaka .............

 Huu ni ujumbe ambao ulifungwa katika ndege ukihamasisha kuondolewa kwa Arsene Wenger

Ligi Kuu England msimu wa 2016/2017 inaendelea jioni ya leo kwa mchezo saba kucheza, mchezo wa West Bromwich Albion ulikuwa ni moja kati ya michezo iliyochezwa siku ya leo ya Jumamosi ya March 18 2017 katika uwanja wa The Hawthorns.

Arsenal ambao kwa sasa wanahusishwa kumuhitaji kocha wa Juventus Massimo Alegri wamejikuta wakikubali kipigo cha 7 EPL msimu huu wakiwa chini ya kocha wao Arsene Wenger ambaye anahusishwa kufukuzwa muda wowote, Arsenal wamekubali kipigo cha goli 3-1 wakiwa ugenini.

Kipigo hicho kinaifanya Arsenal kuendelea kukaa katika nafasi ya 5 katika msimamo wa Ligi Kuu England msimu huu, wakiwa na point 50 lakini mashabiki wa Arsenal wengi wao hususani wa England kwa sasa wameonekana kujikita zaidi katika kushinikiza Wenger aondoke


EmoticonEmoticon