Wanyambo
Wanyambo ni kabila la
Tanzania wanaoishi katika
Mkoa wa Kagera,
Wilaya ya Karagwe. Lugha yao ni
Kinyambo.
wanyambo pia nikabila ambalo lina utamadun tofaut na makabila mengine
katika mkoa wa kagera tofauti zao kitamaduni -mavazi yaliyotumika
kitamadunu yalifahamika kama (embugu)zilitokana na magome ya miti
iitwayo kwa kinyambo "emitoma" Imetawaliwa na viongozi maarufu kama
"omukama" na walio maarufu sana mpaka sasa hivi ni omukama Rumanyika na
omukama Ruhinda Snr(balozi mstaafu) anayekaa makao makuu huko karagwe,
Nyakahanga. Watu wengine wajulikanao ni familia ya Kazimoto walio ishi
Nyakahanga karibu na kiongozi huyo wa jadi. Watu huwachanganya wanyambo
na wahaya kwa kuwa wahaya wana majigambo na maneno mengi sana na hivyo
kuelekea kumchanganya mnyambo na mhaya. Baadhi ya wanyambo
wamechanganyikana na asili ya kinyarwanda kwa sababu wakimbizi waliishi
karagwe na "kuintermarry" na watu wa karagwe. Wanyambo hupenda kula
Ndizi kama chakula chao. Zamani ungemuuliza mnyambo halisi alichokula
angesema "nalya amatoke" maana "nimekula chakula" ila kama alikula ugali
angesema "tinalya akantu" maana "sijala chochote".